Swahili Song Lyrics of East Africa

Bado nipo nipo

by Mwana FA

Bado nipo nipo by Mwana FA

Intro
Wagwan Blood
the personality change, hii ya leo hii!
Hermy

Chorus
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana) x 2
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana?

Verse 1
Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa
Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua
Mi nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia
ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa
napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu
kwani na mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu
watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao
wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao
sioi leo,sioi kesho-kutwa wala mtondogoo
sioi mchana,sioi jioni,usiku wala majogoo
morale nliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa
ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa
eti nizibe maskio
wengine nifumbe macho
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini

Chorus
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo kwanza)
Unasema (bado nipo nipo sana) x 2
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana?

Verse 2
hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?
watu wana watu wao wengine toka zamani
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako
sijui ni dhiki au tamaa tu?
watoto wanaanika njaa tu
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu
msinipe headache staki kufuata Mkumbo
nyi anzeni mi niacheni,staki kufanya gamble
marafiki wanauzana/ndio zao vicheche
na daima wanateteana/usiwaamini usiniangushe
anataka kuolewa na anamegwa kama kawa
demu wako akiuza wenzake,zinduka nae analiwa/yes
staki kuoa sababu staki kulia
najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia
nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi
ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi
alilala na bibi arusi/siku moja kabla ya arusi
na wala sio bwana arusi/bado mnanishauri arusi?
eti nizibe maskio
wengine nifumbe macho
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa

Chorus
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo kwanza)
Unasema (bado nipo nipo sana) x 2
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana?

Verse 3
usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania
watu na akili zao washajichuuza na wakalia
sikatazi watu kuoa
na hata nikiwakataza neno langu sio sheria
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari
inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri
ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari
wanatoroka na wazungu/wanamegwa na vibabu
wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu
ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe
au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe
wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee
haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume
kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria?
sio kila demu umuonae unaweza muoa
eti nizibe maskio!
wengine nifumbe macho!
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi!
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini!

Chorus
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana) x 2
Mwana FA unaoa lini (bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana?

Outro
yes yes it’s yo boy FA
na Hermy B ni kazi chafu but lazima mtu aifanye!
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri!
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari!
yeeeeah, love is love my people
ladies, behave basi au sio?