Bandia
by Pewa Abagenge
Intro:
Eeeeeeh, newskool Genge mzee…..aaah gyea…ahh Pewaaaaaaa Abagengeeee, hehe..
Bcounty meeen
Chorus:
Swagger bandia, Nywele bandia,Sikuhizi kila kitu huwaga bandia,
Mapastor bandia,Mapenzi bandia,weeeeee,we ni bandia?????
x2
Verse 1:
Nlikuwa na beste yangu anaitwaga Kuria,
Ameokoka kila place na bibilia,
Story mtaani alirape ule Maria,
Ameokoka kumbe mkristo,bandiaaa,
Wasanii wengi sana tu ni bandia,
Buda Tomiso noma asana aliimba sinzia,
Mi nko juu naifanya kama career,
Hunaga show we ni rapper,bandia
Ule ex wangu anaitwaga Lucia,
Nlimpenda roho yangu akanivunjia,
Niko single bila manzi nafurahia,
Staki love kwanza zile,bandiaaa
Chorus:
Swagger bandia, Nywele bandia,Sikuhizi kila kitu huwaga bandia,
Mapastor bandia,Mapenzi bandia,weeeeee,we ni bandia?????
x2
Verse 2:
Siendi works mi nafeel tu malaria,
Naenda hosi kutafuta dakitaria,
Bila test anasema dihorea,
Ita polisi kuna doctor, bandia,
Nipeni kura zenu ntawajengea,
Barabara mbili mbili mpaka Busia,
IDP wako tent wanaumia,
Wanasiasa wetu Kenya, bandia
Nimewasha radio yangu nikasikia,
Magorofa zinazama Nairobia,
Waliforge macerti ma engineer,
Elimu yetu pia huwaga, bandia
Chorus:
Swagger bandia, Nywele bandia,Sikuhizi kila kitu huwaga bandia,
Mapastor bandia,Mapenzi bandia,weeeeee,we ni bandia?????
x2
Verse 3:
Naogopa kula food zile za njia,
Masamosa kuna njivaa pia bhajia,
Ulidhani nyama nyama kumbe ngamia,
Kuna butcher zinauza nyama, bandia
Kuna siri ya mabeste ntakuambia,
Kati ya kumi kuna saba wale bandia,
Wakipanda wanazidi kukanyagia,
Sema no kwa mabeste,bandia
Alinipa noti mbili kwanza za mia,
Akasema anashuka pale Chania,
Ninajua pesa sana nikanusia,
Zilikua noti fake yani,bandia
Chorus x4
Outro:
Bandia…….bandia……we ni bandiaaaaa??? *3