Swahili Song Lyrics of East Africa

Binadamu

by AY

featuring Maurice Kirya

Bongo Flava Artist AY

This is A.Y from Tanzania, Maurice Kirya and Hamdee from Uganda.
It’s a dedication to all African who living in poverty.

Verse 1
Usiombee mambo yaharibike.
Pesa usiishike, mfano wa mti upukutike.
Utaonekana si lolote si chochote.
Utaonekana karaha kwa watu siku zote.
Walimwengu hawatakupa mikono.
Magonjwa yatakuvuta ndani ya shimo.
Utakata tamaa, utaandama na balaa.
Pumzi hutovuta kwa raha, kweli usiombee kuwahi.
Survive for fittest; never trust nobody in this world of weakness
Watakukana hata kama ndugu zako.
Watadiriki sema hawajui hutokako
Mama acha kulia, Hayo uliyonayo ni majaribu tu ya dunia. Ipo siku mambo yako yatatulia.
Utasahau hata Mabaya ya zamani uliyopitia ooh hii dunia‚

Chorus
Bagalalinaa, Gendo kole,
You should think about tomorrow
Not only today
Bagalalinaa, Gendokolee
Uuh, Gendokoleee
Yeeeh

Verse 2
Wapo wapi marafiki uliokuwa nao
Enzi zile pesa imekutembelea
Wako wapi sasa? Hawapo wamekukimbia
Sasa huko waliko tayari wanakukandia.
Ada ya watoto hujalipia, kodi ya chumba nayo unadaiwa,
unazidi changanyikiwa. Hata unajuta oh kwanini ulizaliwa.
Piga moyo konde, Maisha uyashinde.
Bado safari ndefu yenye miba na mabonde
Usiweke kinyongo hata kama walikutupa
Remain strong in this world.
Don’t be jealous, Dats all‚

Chorus
Bagalalinaa, Gendo kole,
You should think about tomorrow
Not only today
Bagalalinaa, Gendokolee
Uuh, Gendokoleee
Yeeeh

Bridge
Binadamu sio watu.
Ukiwa na shida hutowaona.
Ona sasa wamekimbia.
Ona sasa wamekimbia.

Chorus