Swahili Song Lyrics of East Africa

Cinderella

by Alikiba

Verse 1
Mara ya mwisho mimi na wewe
Kuonana kipindi kile twasoma
Shule ya msingi kigoma
Najua ulinipenda
Ila hukutaka penzi kulilinda
Ungesema mapema
Iliniuma sana
Mimi leo niko Dar
Aliniyenipenda nishamuoa
Je wataka kumjua jina?
Aitwa Cinderella
Rudi home wewe
Rudi nyumbani
Wasalimie Kigoma
Waambie nishaoa

Chorus
Ulinitesa sana
Sababu nilikupenda wajua
Kijijini kwa bibi Kigoma
Iliniuma sana
Mimi leo niko Dar
Aliniyenipenda nishamuoa
Je wataka kumjua jina?
Aitwa Cinderella
Rudi home ww
Rudi nyumbani
Wasalimie Kigoma
Waambie nishaoa

Verse 2
Hakuna ajuae rangi ya kinyonga
Zaidi ya yeye mwenyewe na muumba
Nami nakujua wewe huwezi ringa
Baby baby
Nakuona u mnyonge sana
Nami nilikuwa hivyo kule kigoma
Usilie kwa uchungu bwana
Imekutachi sana
Mimi leo niko Dar
Aliniyenipenda nishamuoa
Je wataka kumjua jina?
Aitwa Cinderella
Rudi home wewe
Rudi nyumbani
Wasalimie Kigoma
Waambie nishaoa

Repeat Chorus

Verse 3
Uliniadi mapenzi ni kweli uliniteka
Kadri siku zilivyozidi baby ukanitesa
Mami mara uko bize mami
Mi mshamba wa mapenzi
Si ndo wakashare nami
Kila ninapokuona, ninapokuona
Moyo unazima nakumbuka tu Kigoma
Nakosa raha mwenyewe si unaniona
Ila Cinderella kapoza moyo kuchoma
Mmmh! Mi nachoka haki ya mungu
Inga(wa) ni gani kiasi baby najua machungu
Ningetaka kuwa nawe
Ningetaka kuwa nawe
Ningetaka kuishi nawe
Ila tu mm nimeshabaini
Hiyo ni true mami
Nishampata mwingine ambaye anayenifaa

Repeat Chorus