Swahili Song Lyrics of East Africa

Hivi Ama Vile

by Roma Mkatoliki

featuring Stamina

Hivi ama Vile, Roma ft Stamina

Chorus
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule

Verse 1
Stamina: Mimi nampenda uncle Magu mwokozi wa makapuku.
Roma: Ah mimi ukinikata damu yangu ni lowasa mtupu,
So wanangu wa ukawa vidole viwili juu,
Stamina: Hapa kazi tu ikulu mtapasikia tu,
Roma: Hata nifungwe mimi ni Arsenal sio Man U,
Stamina: Hamna lolote ndio maana hamchezi UEFA msimu huu,
Bongo mimi ni Yanga tena vikombe ni tele,
Roma: Ah wapi wanangu wa simba piga kelele,
Ah nampenda snura ana bonge la chura,
Stamina: Mh mm..nampenda shishi mwanamke sura,
Roma: Ah acha ubishi dogo,
Stamina: Acha ligi,mimi amber lulu ndio mkali,
Roma: Mimi Gigy,
Stamina: Eti mziki una team haya team kiba mko wapi,
Roma: Team hazijengi hata wasafi wakijenga masaki,
Mimi wema we boya tu unalipi la kusema?,
Stamina: Mimi zari niko zangu madale na naishi vyema

Chorus
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule

Verse 2
Roma: Mimi mziki ukinishinda mdogo wangu nitakuwa mkulima,
Stamina: Mimi nitakuwa mfugaji nifuge vyote vya nchi nzima,
Roma: Lakini kweli nikila ugali si nitahitaji na nyama?,
Stamina: Basi bifu la wakulima na wafugaji halina maana,
Roma: Ila Ronaldo mkali ki-soccer hana mpinzani,
Stamina: Hawezi kumzidi Messi wakikutana Dimbani,
Kwanza Madrid siwapendi washanichania mikeka,
Roma: Acha soccer huliwezi ka-bet kwenye mieleka,
Stamina: Hivi Ney na Madee nani raisi wa manzese,
Roma: Hata udiwani hawafai,kwanza mmoja ana kithethe,
Nisha zunguka nchi nzima kila kona ninashabiki,
Stamina: Acha uwongo hivi ushafanya show kibiti,
Roma: Madereva tunaleseni makonda mnatupa loss,
Stamina: Mbona makonda hatuna vyeti ila tunaaminiwa na boss,
Ila wewe bwege ukimuacha mama Ivan utapata dhambi,
Roma: Walahi! nishaweka kambi ninampenda Mange Kimambi

Chorus
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule,
Stamina: Hivi Ama vile,huku ama kule
Shangwe nyingi ziko wapi roma huku ama kule,
Roma: Zinanichanganya sijui ni huku ama kule,
Maana ninazoskia huku ndio ninazo ziskia kule

Outro
Roma: Hehehee..Ila mdogo wangu wewe unapenda sana Ligi wewe,
Yani wewe unaweza ukabisha mpaka outro wewe,
Kwa mfano mimi kama mimi yani,
mimi nakumbia namkubali Mussa babas wa babas,
Stamina: Wai…kimpango wako bwana wewe,
si unajua watu wafupi,afu si unajua tabaka la morogoro,
Mimi namkubali chief Kiumbe wewee,
Roma: Hahaa