Swahili Song Lyrics of East Africa

Mabinti

by Mwana FA

CHORUS
Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!

Wengine ndani jeans wengine ndani ya skirt
Wengine mini au magauni ya vitambaa vyepesi
Mradi istizahi wanipore uhuru wa nafsi
Weledi wa ajabu kwenye mambo ya chini ya paa
Kuna werevu wa ajabu kwenye mambo mengi bar
Hawanipi shida sio balaa
Na zaidi nawapenda mabinti watundu
Mapozi ya kichokozi au sio pozi vurugu
Mitindo ya kiyahudi hijabu zikatazo kichwa
Na mikogo ya kifisadi sio mmakini inapotosha
Unaona shanga za miguu naita vikuku
Ingawa wenye ufahamu nipotofu
Watoto wa ki9bongo hakuna mchezo
Kuna walatino waafrika na wasanta domingo
Kuna mpasua toka chini mpaka kando ya kiuno
Milango wazi kwa yeyote aliye na mdomo
Sijapoteza macho ya kuangazi warembo
Nakosa uzalendo nionyeshwapo miguu
Napata uchizi wa mtima
Choma fedha na muda sioni balaa
Natumai sifunzi hasaraa?
Ni hadithi na sio biashara
Ukishindwa Inshallah

CHORUS

Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!

Kuna kifua kama cha zay B
Kiuno kama cha Ray C na pozi Jay D na sauti kama Fina
Au labda ya aunt Ndina ipo njema matabasamu
Kama binti Maumba wa kino Msio nidhamu
Mtafanywa mpende ngono Hold on!
Kuna pozi za kimtoni kama Tausi Likokola
Unataka ni full bakora mabinti wangali wanang’ara
Warefu warembo kama twiga mithili ya Happy Magese
Midomo kama ya Shose
Utapenda uonekane yaani viwanjani ututese
Au binti maarufu utasema Aina anatosha?
Kama nnataka mwanya nafahamu wapi ntaupata
Mwite Aminata wa keita
Binti wa vigogo unamtafuta Mboni Mhita?
Mwili utakaokufanya upende love kama wa Mercy
Na macho yanayovuta kama ya Miriam wa Ikoa
Unaweza utangaze ndoa
Wengine mziki kama Shanice
Au kama connie stephans
Naiota rangi ya Caroline na lugha tanu kama ya Seven
Najua mnawaita masister Du! bendera hewani
Sometimes wavute widdy Mentally japo wazuri
Mithili ya Kibibi
Miondoko kama Faudhia
Au ungependa kithethe mithili ya Radhia
Watoto wa shule wassiwafanye mpagawe
Ilhali kuna wenye haiba kama Halima Bandawe
Mi kwa mabinti -nisahauliwe

CHORUS

Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!

Kuna mabinti wapo kamili kila idara familia bora
Akili zisio lala maumbo bomba na sura
Kuwapata ni full Gospel wao ni ajira na hawaitaji zaidi ya sera
Kuna mitego ya khanga mambo kitanga
Kama una jichohii unapaswa kuwa umeiona
Michirizi ya utamu nyuma ya goti mimi hoi
Una moyo hai hili sio toi pigo jingine kama Sunset
Ubishi haufai ona visa kwenye mitindo ya vichwa
Anuani pepe za mitandano na simu zinawehusha
Ukitaka upgawe njoo kiwanja
Jaribu kuwa mkweli nionapo vitovu wazi hakuna si mahututi mimi
Kuna wadada, wamama, masister du wote wapenzi
Wana nataka staki sio kamanda naachia ngazi
Omba majina Amina kawa Amayna, Naima ,Clara na Rayyah!
Kuna Tayana,Aneth hata bongo kuna Aaliya?
Candy, Nicole, Uenice au labda Marayah
Sikitu hataki jina na Asia anaitwa Eshia
Pamba hazibani ni hatari
Ni makusudi tuone mstari wa kufuli mambo ya kivazi
Wachumnba wote mpo pina wote funga kazi
Msiache washkaji wawafanye watumwa nyia ndio mama
Anayewaponda apate laana

CHORUS

Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam, kweli kweli
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh!