Mac Muga
by Alikiba
Verse 1
Mcheza bongo Mac Muga
Yuko single sana Mac Muga
Ukimwona mtu akijinamia kwa sababu ya maisha yamchanganya
Chali wangu alizamia
Kuenda kusini mwa Africa
Huku pia akimchanua kwa sababu ya maisha aliyofuma
Alikuwa maarufu sana,
Akajiona yeye ndo winner
Kwa kujichanganya na wasichana
Club zote za huko kujulikana
Yeye Mac Muga
Wewe Mac Muga
Ah, hii dunia,
Mac Muga huruma!
Chorus 2x
Mungusha asumani alipofika South Africa alikuwa na maisha bora
Ya juu, ya thamani tena yanayohitajika magari yote kwa nyumba
Mbona sasa amesharejea, hajui wapi ataanzia!
Hakuna kazi mtu akajinamia
Mac Muga hii ni dunia
Verse 2
Akajichezea, gari ya kutembelea
Shida walimwelezea wasichana na shida zao akawatatulia
Wewe upewe nini Mac Muga
Mungu akupe nini Mac Muga?
Nyumba ulijijengea, foro kuta nyumba
Wewe ndio wewe, wengine fala!
Wewe, Mac Muga
Mbona sasa umeshatimua!
South Africa wamekutimua
Na sasa home usharejea
Wewe Mac Muga
Mungu akupe nini Mac Muga?
Chorus 2x
Mungusha asumani alipofika South Africa alikuwa na maisha bora
Ya juu, ya thamani tena yanayohitajika magari makubwa, nyumba
Mbona sasa amesharejea, hajui wapi ataanzia
Hakuna kazi mtu akajinamia
Mac Muga hii ni dunia!
Verse 3
Yipes kana huoni kwa Mac Muga
Woi noma huruma kanyongo’nyea
Afanye nini sasa, cha kufanya
Kila anachachofanya anaona anakosea
Yikes, kama huoni kwa Mac Muga
Woi noma huruma kanyongo’nyea
Afanye nini sasa, cha kufanya
Kila anachachofanya anaona anakosea
Akiwa jambazi akili zake zitaishia
Akiwa mwizi anaona atauliwa
Akifikiria kujiua
Nafsi yamzusha basi analia
Wewe Mac Muga!
Mungu akupe nini Mac Muga?
Wewe Mac Muga!
Basi upewe nini Mac Muga?
Mungu alikuzawadia
Sasa ushachezea!
Wewe Mac Muga !
Basi upewe nini Mac Muga?
Mungu alikuzawadia maisha
Sasa ushachezea!
Haya, haya,
Wangu Mac Muga
Msela hao
Wa mpani huna
Wasee wa maskani wanakukimbia!
Mac Muga noma
Hee! Mac Muga
Skonde, upige moyo konde,
Mac Muga!