Mulika Mwizi
by Kidum
featuring Sana
Verse 1
Ukiona mwanaume kwa hali ya kulia, jua yakwamba ameguswa pahali,
Sio rahisi, si kawaida kushuhudia mwanaume akitoa machozi,
hapo zamani nilidhani mwanaume akipoteza kazi ndio uchungu, ndio unyonge,
kumbe mapenzi ndio sumu kali, inayofanya mwanaume kulia, kama mtoto mtoto, kama kidogoyo,
hapembelezwi, hanyamazishwi, machozi yake inatoka ikienda tumboni
hapembelezwi, hanyamazishwi, machozi yake inatoka ikienda tumboni
Chorus
Mulika mwizi, mulika na tochi, mulika
Mulika mwizi, kama kuna giza mulika,
Nimulikie mwizi, nasumbuka, nataka kujua nani mwizi wa mapenzi
Verse 2
Barua pepe kwa simu ya rununu, ujumbe mfupi unafutwa na sekundi tatu (sekundi tatu),
Nilimpenda baibe wangu, nikampea roho yangu, amechukuliwa, amenyakuliwa,
Kama fulani hapa mtaani, mwenye magari, na mapesa, amechukua baibe, ikanifanya crazy,
Sipembelezwi, sinyamazishwi, machozi yangu yanatoka yakienda tumboni,
Msiomboleze, mnamujua huyu jamaa, kajifanya bubu, wengine vipofo
Chorus
Mulika mwizi, nimulikie mwizi,
Nimulikie mwizi, nasumbuka, nataka kujua nani mwizi wa mapenzi
nani mwizi wa mapenzi
Verse 3
Ukiona baibe wako anaingia kwa bafu na simu mkononi, huyo ni mwizi (mulika mwizi)
Uniona mzee wako anazima simu kila mara akiwa kwa nyumba, mulika mwizi (mulika mwizi)
Oh Oh Oh Oh Ohooo
Oh Oh Oh Oh Ohooo
Nimulikie mwizi jameni, (mulika mwizi)
Mulika mwizi, nionyeshe, niambie ni wapi,
Nimulikie mwizi, mwizi wa mapenzi, mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)
Nani mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)
Nani mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)
Waniua, waniumiza (ohooo)
Mulika na tochi, natazama mbele si nyuma, mulika mwizi,
kila mtu mwizi wa mapenzi, kila mtu mwizi wa mapenzi,
pia mimi mwizi wa mapenzi