Swahili Song Lyrics of East Africa

Natamba

by Aslay

Natamba by Aslay

Intro
Natamba by Aslay
Natamba natamba
aaah!

Verse 1
Kilichonishawishi upole wako
Na heshima yako
Wazazi wangu wamekusifia sana
Kwa tabia yako
Sura yako ya upole
Inanivutia aaah
Shape twiga mwenda pole
Najivunia 
Oh tupeane mapenzi iwachome
Eeeh na kama number waisome
Hata tukigombana wasione
Washike jembe wakalime
Mapenzi mazuri
Wakutane wawili wanaopendana
Usizidishe washauri
Watasabisha tuje kugombana
Aeeeh

Chorus
Aee angalia shape
Kama wema sepetu
Angalia jicho
Hamisa Mobeto
Ka rangi kake
Elizabeth Michael
Yani we mrembo
Wallahy nachukua jiko
We ndo wangu wa milele

Verse 2
Nauza dagaa ili ninunue motokaa
Nikuridhishe
Unanipa furaha na nguvu ya kusaka
Chapaa nisikuangushe
Una nyota ya adamu na hawa
Ooh tunavyopendana
Hata wakituchukia ni sawa
Ooh tuwaminyie mama
Wanaona umenipa dawa
Ooh wanaongea sana
Chunga usije kuota mbawa
Ooh ukaniacha dilemma

Natabiri pweza penzi
Litafika mbali
Nacheka kingereza
Ndo maana nacheza
Ya watu natupia mbali
Natabiri pweza penzi
Litafika mbali
Ndo maana nacheza
Ya watu natupia mbali

Basi babe nikumbatie aah

Chorus
Aee angalia shape
Kama wema sepetu
Angalia jicho
Hamisa Mobeto
Karangi kake
Elizabeth Michael
Yani we mrembo
Wallahy nachukua jiko
We ndo wangu wa milele