Nini Dhambi
by X-Plastaz
All my people
East Africa
Tanzania, Uganda and Kenya
Dar es Salaam, A town
Wherever you are
Piga magoti, tuombe Mungu
Hii ni siasa, dini, vita, ubwana, utwana, au kiama ghalika, sodoma na gomora?
Simama imara, zunguka kila kona, kila anga angaza
Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia
Na hapo ulipojishikiza g’ang’ania, sikilizia, vumilia baadae usije jutia
Hii ni mahususi na maalum kwa watu wangu
Walemavu, vipofu, zeruzeru na wendawazimu
Watoto wa mitaani, fukara, masikini na wenye akili zao timamu
Hii kamba ngumu
Mjue tunavutana na wenye nguvu
Vitambi na mashavu
Hakuna tena fair game
Refarii kauzu
Uwanja wenyewe mkavu
Ujira mgumu, malipo finyu
Kilichobaki kucheza rafu
Tumechoshwa na ukabaila, ubepari na ubeberu
Wakati ndo huu
Ukombozi ndo huu
Na sasa naamuru mliopo chini wote mpate divai ya vinibu
Mtetezi wenu nikaze gidamu
Nimwage sumu ya upupu juu yao
Wajikune bila aibu
Kwanza saluti kwa waliyotangulia kuzimu
Pili tuombe Mungu
Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku
Utujaze nguvu
Tupate kudumu ndani ya game
Tutakapofika kuzimu siku ya hukumu
Utupe nafasi tupate kutubu
Kwani tunajua tunatenda maovu
Tunakula haramu
Tunatumia kila mbinu
Juju, uhalifu, upanganyifu
Ili tuweze kujikimu
Lakini isiwe kisingizio kwa wanadamu wengine kunyimwa haki zetu
Kutuzibia riziki zetu
Kutuita makafiri, dharau na kutukashifu
Kwani nini dhambi
Chorus
Nini dhambi kwa mwenye dhiki,
Kipi haram, kipi halali,
Kila mmoja anaitaka hii riziki
Kitendawili, vurugu mechi
Huwezi tabiri
Kwa nini?
Uliza swali, kama sote tungekuwa wasomi, matajiri
Ni nani angelifanya kazi za kutisha na hatari mfano ya mochwari
Kila mmoja wetu hapa mjini kaja kwa dili
Kila kitu, kila mahali
Na hata ngozi ya mtu dili
Wengine wachawi, waganga feki
Matapeli, wasafiri kafiri
Wakati wengine wapole kama walokole
Mchana pirika nyingi maofisini
Kumbe night kali, kahaba
Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri
Ah!
Wapo waliopoteza maisha katika kufight life
Kumbukumbu zao zimebaki makaburini
Na wapo waliopoteza kabisa tumaini la kuwini
Hao roho zao utadhani wamezitoa rehani
Wakikutight mahali fulani
Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi
(Chorus)
Kweli Bongo kutafuta braza
Utajajuta utakapojikuta huna hata bukta
Shauri yako we tegesha tu kama golikipa
Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa
Huna elimu, hun fani
Lakini nguvu, ulimi, uchumi unao unaukalia
Kumbuka
Kupata au kukosa yote ni kawaida
Sometimes unalala unaota unakula
Unakunywa, unapiga denda
Na kula uroda na demu bomba
Ukikurupuka tu unakuta patupu
Hakuna kitu