Swahili Song Lyrics of East Africa

Nitampata Wapi

by Diamond Platnumz

Nitampata Wapi by Diamond Platinumz, lyrics of song

sura yake mtaratibu mwenye macho ya aibu
kumsahau najaribu ila namkumbuka sana
umbo lake mahbibu kwenye maradhi aliye nitibu
siri yang kaharibu bado namkumbuka sanaaa
 
aliye nifanya silali jua kali nitafute tukale
lakini-(ila) hata kujali, darling, akatekwa na wale x2
ntampata wapi kama yule niliye mpendaga sana
ntampata wapi kama yule anipende sana x2
 
ai nyotaaa nyota ndo tatizo langu, nyotaa mpaka nalia peke yangu
ai nyotaaa nyota ndo shida yangu, nyota wamenizidi wenzangu
alidanganywa na wale wenye pesa nyumba gari mi kapuku akunijali akanikimbia
alidanganywa na wale wa mapesa nyumba gari mie ungaunga akunijali akanikimbia
 
aliyenifanya silali jua kali nitafute tukale
lakini hata akujali darling akatekwa na wale x2
nitampata wapi kama yule niliyempendaga sana
nitampata wapi kama yule anipende sana x2
 
bado ananijia ndotoni ila nikiamka simwoni
bado ananijia nikilala haki ya mungu sio masihara
bado ananijia ndotoni nikiamka simwoni
bado ananijia nikilala haki ya mungu sio masihara
 
Hii ni sauti ya rais
ilomshindaga ibilisi
kwa wanadamu sio rahisi
 
Kamwambie
lazima ujue kutofautisha
kati ya msalaba na jumlisha
kuna X na kuzidisha
 
bado ananijia nikilala
haki ya mungu sio masihara