Pete
by Ben Pol
Verse 1
Hadithi ya penzi langu umenikata nini mwisho
huthamini huoni pendo lako nalihitaji leo kesho
nishawahi kukosa, mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi, nishawahi kukosa
nasema niliteseka mchana na usiku mimi
nishawahi kukosa, mwenzenu nilisumbuka
mchana na usiku mimi, sitaki tena kosa
najua nitateseka
mwisho sitokuwa nawe tena naulizaa
Chorus
Kama pete yangu, inakuchomaa kidoleni
ni kama pendo langu, linakuchoma moyonii,
bora kuitoa aaah aah,
pendo kulivua aaah,
bora kuitoa,
moyoni mwangu mi nisiteseke
bora kuitoa aaah aa,
pendo kulivua aaah,
bora kuitoa,
moyoni mwangu mi nisiteseke
Verse 2
sikujali wambea wanafki walosema
hatutadumu mimi nawe tutajaachana
wakiniona siko nawe si ndo watasema
hata nyumbani watajua tumefarakana
nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia
maana bado nakujali, kwako nilishatua
nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia
maana bado nakujali, kwako nilishatua
kila jema n'tendalo mie, kwako limekuwa sio
nitakapo kujua ulipo, wanijibu utakavyo
pete kidoleni mwako, yanisuta mwenzio
ndo maana nikukosapo, moyo wanienda mbio
Repeat Chorus till fade