Swahili Song Lyrics of East Africa

Propaganda

by Fid Q

Fid Q from Tanzania

Verse1
Machungu unapozimwa,ili ufunikwe na asiyeweza
Mbaya zaidi wanampa Promo halafu kwenye Show unammeza
hautaki kuwa tatizo sababu unaweza tatuka
hauwezi jua wapi nitatua ka Jiwe gizani likitupwa
wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua/hamkomi?
igeni nione jinsi msamba mnaupasua
hivi mnaishi ili mle au mnakula ili muishi?
kumbuka a small leak will sink a ship
mazingira hatarishi, Mabwana afya wanamaPesa Mob
uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo
ogopa kuoa haraka kama unaogopa talaka
na ukivote in a hurry ujue unaproduce corruption
maneno yao ni matamu lakini midomo yao inanuka
ukipewa usisahau,ukitoa TOA bila kukumbuka
usihofie kupitwa ilimradi muda haukuachi
amini kesho itafika kama ipo ili uipate
tunachukiana kwasababu tunaogopana
tunaogopana kwa sababu hatujajuana
hatujuani kwasababu tunatengana
dunia ni nzuri.. walimwengu hawana maana

Chorus
Polisi wanasapoti Gangsta Rap ”ili uhalifu uongezeke”
Wabana pua kuimba mapenzi ”je itafanya ukimwi usepe”
Media zinapromoti beef ”wanadai zinakuza mziki”
Wadau wana wasanii wabovu ”nyie wakali mtatoka vipi?”
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?
saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda
yule last King of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda

Verse2
Polisi huniita Mzururaji na wanajua mie ni MC
Kisha hunipa ishara kama wanavuta uradi kwa Tasbih
Baya lisilo nidhuru ni Jema liso na faida
nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha
kuanzia Kata,Tarafa,Wilaya,Mikoa hadi Ngazi ya Taifa
nikifa siachi Skendo, ninauhakika nitaacha Pengo
kwa hivi vina hata Wakulima hujikuta wanameza Mbegu
pia ni kama Liberation struggle machoni mwa Chegu
ukiwa mkali ka Marco Chali.. raia watafeel tu
wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu
rafiki sio urafiki usipochanganywa na Kazi
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi
haupaswi kumuamini Muongo hata kama akiongea Ukweli
ni Dhambi kutumia Dini kama njia ya kututapeli
wanajiingizia kipato kwa kimvuli cha misaada
hawatufunzi tuwe Viongozi labda Viongozi wakuwafata
utata huja, tunapoanza kuwachunguza
badala ya kuwafata ndipo Siri zinapovuja
tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda
kama umevutiwa na Asali, jiandae kumkwepa Nyuki
hauwezi kumtisha kwa Mawe Adui aliyeshika Bunduki
ni uchunguzi tu wa Kisayansi ambao haukufanikiwa
kama ule wa Ng’ombe kula Nyasi tu halafu anatoa Maziwa

Chorus
Polisi wanasapoti Gangsta Rap ”ili uhalifu uongezeke”
Wabana pua kuimba mapenzi ”je itafanya ukimwi usepe”
Media zinapromoti beef ”wanadai zinakuza mziki”
Wadau wana wasanii wabovu ”nyie wakali mtatoka vipi?”
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?
saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda
yule last King of Scotland si