Swahili Song Lyrics of East Africa

Siri ya Mchezo

by Fid Q

featuring Juma Nature

Siri ya Mchezo lyrics, by Fid Q featuring Juma Nature

Verse 1:
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo
sikuwa na umuhimu kihivyo stimu zikanipa elimu ya Biko
Kimaandiko kimistari.. hadi fans wanascream nikirap..
sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop
 
Wanapagawa. Na baadhi ya mambo nayoyajua..
pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz 
Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz
 
haileti bingo, mshiko? Star ishi simple
sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo
wanaodharau.. hujiletea matatizo..
hawajui kama wadau hupendelea kukuona hivyo?
 
bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu
jikombe ugongwe mtaaa ukuone hauna ishu
ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa
mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda
 
Usmati anaotinga, majumba mandinga
ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji
na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati
 
sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu
kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu
Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA..
baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA
 
NYUMBANI nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI..
najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?
labda kubisha na wakinitisha najihami..
inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani
 
Pole MAPROSOO( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu..
WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu
na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu
 
kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu..
huo ni utumwa pia
Unafanya vijana wanaumia..
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..
 
 
CHORUS: (Juma Nature)
Siri ya mtungi aijuaye kata..
komaa kaza.. kisha utapata x2
Siri ya mchezo naijua mimi..
tu.. na hakuna mwingine x2
 
 
Verse 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma
wakati SIASA kila mara ukiwa unang'ara ujue kuna.. kinara
anayeunda msafara wa wanaojituma
na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna
 
KIDUMU CHAMA CHA MASELA Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,
tuone kufuru za wenye hela
TANZANIA ni demu wa mtungo wanamuiita CHA WOOTE
HANGOVER .. anaikimbia kwa kupiga mtungi saa zote
 
Mkubwa anazuga atasolve matatizo ya nchi yake
na gari bovu.. halisukumwi kwa kukaa ndani yake
MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza..
je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza?
 
hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion
na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions
CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically..
hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free
 
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu
kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua?
zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
 
Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka
Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA
Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka!?
 
CHORUS: (Juma Nature)
Siri ya mtungi aijuaye kata..
komaa kaza.. kisha utapata x2
Siri ya mchezo naijua mimi..
tu.. na hakuna mwingine x2