Swahili Song Lyrics of East Africa

Starehe

by Ferouz

featuring Professor Jay

Starehe by Ferouz featuring Professor Jay

Chorus (Ferouz)
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani
Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Sua side Scott Jenta kwaherini
Bongo Record na Majani kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Makongo na Jiteute, kwaherini
Mohaa na Azania, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa
 
Verse 1 (Ferouz)
Saa saba juu ya alama saa nikiitazama
Nimeshaachana na Jack sasa namfata Salama
Saa kumi na mbili na appointment mademu wawili
Achana na Lily ambae tutakutana saa mbili
Jenny wa Mikocheni ambae sasa hayupo tena duniani
Aliyekuwa akinisubiria pale Vatcan Kijiweni
Amina na Semeni tunakutana kwa Macheni
Na kila siku nawabadilisha tena kwa foleni
Huo ndio uliokuwa mwenendo wa maisha yangu
Mimi viwanja kujivinjari na machangu oh ooh
Niliona fahari ii yeah
Starehe mi nilizifanyia papara
Nilibadili mademu kama vidaladala
Nikienda nimepanda hili, nikirudi lile
Nilitamani starehe zote nizitawale
Hata kumkumbuka Mola wangu ilikuwa ndoto
Nilitekwa na ulimwengu kumbe naukimbilia moto
Katika kubadili wasichana nilikubuhu
Nilitembea na watoto wa geti, machangu na masista duu
Ubaya kwamba condom sikuitambua
Kwa kujua kwamba ladha ya mapenzi itapungua
Kumbe nilikuwa ninapotea njia
Niliyoshauriwa mimi niliyapuuzia
Idadi ya wanawake ikawa lukuki
Ikafika kipindi wengine nikawa siwakumbuki
Ona, ona aa
Ona sasa yaliyonisibu kwa dada yake Bashiri
Nilishamsahau kama tulishakutana kimwili
Nilivyomuona, nikamtongoza tena
Tena kwa mara ya pili
Ona sasa aa aah
 
Chorus (Ferouz)
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani
Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Afande Sele Morogoro, kwaherini
Arusha wanaapollo, kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Discipline Camp na Wakushi, kwaherini
Sinza Star na Choka Mbaya, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa
 
Verse 2 (Professor Jay & Ferouz)
Kijana vipi mbona hujagonga mlango
Jipange kwenye foleni mmoja mmoja ndio mpango
Ondoa mashaka, tiba bora haihitaji haraka
Subiri watibiwe wenzako nawe utafata
 
Dokta mi nimekuja kufanya hitimisho
Naamini hii ndo itakuwa nngwe yangu ya mwisho
Dalili zinaonyesha nimeathirika
Ila nimekuja pima tu nipate uhakika
Hebu cheki dokta nilivyokonda
Nimebakia mifupa, mwili umetapakaa vidonda
Vipele usiseme hii dalili ya umeme
Dalili ya umeme eeh
 
Oh acha uoga hata malaria hiko namna hii
Unaweza ukakonda kwa typhoid au TB
Ukinificha unahatarisha maisha
Ni bora kubainisha kipi kinakutisha, eeh
 
Homa za mara kwa mara kwangu hazikatiki
Kuharisha, kutapika mara 62 kwa wiki
Eh angalia hata nywele zilivyonyonyoka
Mabeba yamepanda juu utasema yanachomoka
Ninao, ninao
(Subiri vipimo)
Ninao, ninao
(Usikate tamaa)
Ninao, ninao
Dokta usinipe moyo
Ni sawa unampa mfupa autafune kibogoyo
Duniani mimi sina umuhimu
Kuiga dunia napaswa inanilazimu
Ni bora nijue tu nielekee kuzimu
 
No, no, hayo maamuzi ya ajabu
Na ni ulimbukeni kujiua pasipo sababu
Maradhi ni kawaida kwa binadamu hilo ufahamu
Ni vyema ungetulia upate majibu ya damu
 
Sasa kumbe we unaona mi nasubiri nini?
Ni bora tu niwahi kupumzika kaburini
 
Starehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya
Wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya
Vipimo vinaonyesha ni kweli umeathirika
I’m very sorry kupoteza nguvu ya taifa
Ni vyema kufanya ibada na kumrudia Muumba wako
Kula vizuri, fanya mazoezi, pumzisha mwili wako
Ukizingatia haya utaishi kwa matumaini
By the way, unayo nafasi hebu jiamini
 
Mbona aliyeniumba sasa nishamkosea
Hata ardhi na mbingu vyote vinanizomea
Malaika wa adhabu kwa hamu wananingojea
(Koh koh koh)
Nikifika huko nani atanipokea aah aa
 
Chorus (Ferooz)
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani
Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Wa bara na visiwani, kwaherini
TMK, Kino Graid, kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!
Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Kikosi Cha Mizinga, kwaherini
Migo Migo, Sinza, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa