Swahili Song Lyrics of East Africa

Tamaa Mbaya

by 20%

Sifa ya moyo tamaa, moyo sifa yake kutamani
Tamaa ya moyo, inaweza kukuweka matatani
Unatamani kuzaa, wakati bado uko shuleni
Tumia akili kukataza, kabla hujawa matatizoni
Ile ndoto ya kitandani, achana nayo
Kama unahisi labda haiwezekani, kuendana nayo
Unaweza ukaota umejenga angani, angani
kuhifadhi ndoto ya shida gani, wewe.

Chorus
Tuliza moyo wako, kubali mapungufu yako
Rahisisha mahitaji yako, ongeza kipato chako
Chunga tamaa mbaya x4

Sifa ya macho kuona, kutazama kinachoonekana
Ila sio kila unachokiona, utadhani kupata inawezekana
Nyumbani kuna msichana, njiani utaona wengi wasichana
Bora kuishia kutazama, kuliko kujifanya unaweza sana
Siri ya maisha yako iko kwa muumba, muumba
Alisema mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba, kuwa simba
Hawezi kuongea, eti anaforce kuimba
Bora kutulia ama kupiga marimba, utasikika pia

Chorus

Mwanzo wa safari nakufuata kijana
Nakuja na swali unipe jibu la maana
Dunia bila wizi hivi itawezekana
Kama haiwezekani siku tukijaonana,
Nitakiweka mbali kisimu changu cha mchina
Vijana wote nitawaona hamna maana
Tunarudishana nyuma mambo ya kuibiana
Mwenzenu naona noma polisi kupelekana yeah

Chorus