Swahili Song Lyrics of East Africa

Usijaribu

by AY

AY from Tanzania

Intro: Let me talk to ya! Nataka kusema sana (No si sana) kuhusu watu wa aina
fulani, mzeiya A.Y sema

Chorus.
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba x 4
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao x 4

Verse I.
Yatazame vyema macho yangu right now,
Nishapitia mambo mengi hata zaidi yao.
Unapong’ata kwangu na kupulizia kwao,
Unapochoka zaidi baada ya kuona mi nacheka nao.
(Oh) Leo nakupa ukweli baada ya kuona unanispy,
Cheza nami mbali sitaki hata unisabahi.
(Sikujui) Niaje nipoteze muda nikuchunguze,
(Hunijui) Vipi utunge uzushi kwangu uyasambaze.
Mind your business hujui style ya Maisha yangu,
Basi sitaki ubishe hadi kwenye anga zangu.
Kila siku unayafuatilia, nayoyahangaikia,
Lakini huwezi kuniharibia.
Usione nimeshhh ukataka kupima,
Nilikuona mwema kumbe zzzz nishakusoma.
Nikiwepo mtu poa, nikiondoka unanichoma,
Sasa unapochoma kama unaoga nje mchana ah.
Niko imara zaidi ya chuma cha pua,
Sitabiriki ujio wangu moyo wako unajua.
Mlango wa ngome yangu mjomba noma ngumu kuingia,
Ndo maana bado mi nakamua border nyingi napasua.

Bridge.
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
OYAA X 2 (OYAA X 2)

Chorus.
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba x 4
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao x 4

Verse II.
Usione watu wamechill wametulia, Busy
Basi ukaona easy kuwachezea, ukidhi.
Kupandikiza chuki news kudandia,
Please, sitaki lawama kama vipi we potea
Fanya usepe tu kwangu, kwangu hupati kitu fool
Niogope kama OGOPA full wa mbuzi kama FID Q
(A.Y x2) Bado nafanya mema huh
Nikipata, nikikosa namshukuru Mungu tu,
Kikulacho mbona kinguoni mwako.
Wanaokuua mbona wa karibu yako,
We unashangaa nani anauza file lako.
Kama Adili kama mi (Bora niwe peke yangu).
Deal zako ka zinabuma basi hasira usilete kwangu.
Kama zali oh si lako jitume kibingwa wangu.
Sio unakaa tu, kazi tu, kupiga majungu.
Napo muda unapata bado unapiga virungu.
Mchawi hana alama wapo (humuhumu).
Asiyependa uendelee ni (mchawi tu).
Hakosi uja kwako hodi kila saa (Ngo,ngo)
Ndani chuki nje kila saa anakupa tano. (Ngum, Ngum).

Bridge.
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
OYAA X 2 (OYAA X 2)

Chorus.
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba x 4
Aah juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao x 4

Bridge
(Aaah) Usijaribu kuchunguza sura hii
(Aaah) Kama ina raha ama zzzz
(Aaah) Usilete tabia za kizamani.
Maisha yangu yanakuhusu nini

Outro.
Au vipi bwana , Ni hayo.
Huu ni muda na kila mtu kujiheshimu rafiki yangu.
Haijalishi wewe ni nani na unatoka wapi.
Niachie mimi nifanye kama mimi.
Sababu siwezi kufanya kama wewe na wewe huwezi kufanya kama mimi.
Sikiliza Ambwene, hili ni bonge la dude, bonge la beat kutoka kwa OGOPA.
Matrack kama haya yanatakiwa kusikilizwa mtaani. Chuki kibao zipo, kwa nini?
USICHUKULIE POA X 2