Swahili Song Lyrics of East Africa

Wazo la Leo

by Stamina

featuring Fid Q

Intro
U know what majani?? Nice to meet you Homie
Its MORO Town Baby,,, SHOROBWENZI
 
Verse 1 (Stamina)
Elimika Nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu
Hip hop haijengwi na bifu,underground usijaze fomu
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku hizi hazioti
Maisha njia panda,mtembezi chagua pa kwenda
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe suspenda
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha ushamba
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga
 
Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
 
Verse 2 (Stamina)
Underground panga tenzi,ustar hauji kwa promo
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku punguza ngono
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba
Mapenzi yakikusumbua,tafuta daktari wa kitanga
Vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndio disegner
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna
Dunia duara,jitahidi uizunguke
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke
Huna undugu na bakhersa,niaje aje unakula unga
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi
Mwambie na dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje kupewa
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe salamu,the great braza kanumba
Mwambie bongo sio tamu,na lulu bado wamemfunga
 
Chorus (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
 
Verse 3 (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza
Nchi tayari imekonda,mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri,jipange kuikwepa hasara
kijana vazi la msuli,haliwezi kukuvisha busara
ukiishi kwa hisia,kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia,ujivue kuwa mtanza
kata ya kijiji,haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji,msuli ukishuka kimeo
uchumi umeshika tama,kwenye shavu la mlanguzi
raia usilaumu chama,shiriki kwenye uchaguzi
unaweza ukavaa kinga,ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga,sambaza ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa,ukiwa nae fanya vya maana
akiondoka atakutesa,utamsaka usiku na mchana