Swahili Song Lyrics of East Africa

Wewe

by Angie

featuring Chidi Benz

Hakuna asiyetamani kuwa na mwenza kama wewe,
Hakuna asiyefurahi kuishi nyumba moja na wewe,
We kunipenda nafurahi kwa wenzangu najidai,
Ukiwa mbali natamani nikufuate

Chorus
wewe wanipa sababu ya kuishi,
sijali kama huna mali,
lazizi nifanye niwe wa milele x2

Nimechagua kuwa na wewe,sijali kama huna money,
Napenda unavyonipenda,usiniache peke yangu,
Nipe mapenzi yote usinibanie,
Twende kwetu nyumbani,nikakutambulishe,
Niahidi kuwa ma baby pamoja tuzisake iyee iyee,
Kwa shida na raha,daima,uwe mine,
Kwa vita na njaa tusiachane hata iweje

Chorus
wewe wanipa sababu ya kuishi,
sijali kama huna mali,
lazizi nlfanye niwe wa milele x2

Nipe chochote popote
karibu nawe nikianguka niokote sikuachi nipe vyote
vyote vyote kisibaki chochote
Najua kama unanipenda sana
sana sana leo zaidi ya jana
sana sana ile ya kukamatana
sana sana yaani hatuwezi achana
usiwe na hofu kwako mi kipofu
usiwe na presha ukae ukikesha
labda univizie tym ninayojirejesha
jiamini niwewewe tu unayeninogesha