Yule
by AY
Intro
Aha (2x)
Umeshaisikia hii?
Kutoka kwa A.Y
Chorus 2x
Yule
Nampenda sana jinsi alivyo
Yule
Nampenda sana jinsi alivyo simple
Yule
Nampenda sana jinsi alivyo, nitafanyaje?
Patamu hapo
Verse 1
Anavyotabasamu ndipo anaponipa hamu
Sura umbo lake basi lanipa wazimu
Nataka kumfuata, nahisi atakataa
Naogopa akinimwaga, story zitazagaa
Napenda miondoko yake, tabia yake
Umaskini wangu utanifanya nisimpate
Yule, anayesumbua akili yangu
Yule, anayeumiza moyo wangu
Najua hafahamu, najua hafahamu
Moyoni mi nabaki na mawazo
Lakini kumwambia ndo siwezi
Chorus 2x
Verse 2
Tatizo hajui, bila penzi lake maze sijitambui
Mi nitafanyeje, hata nikimuona mdomo unajaa mate
No no no (2x)
Napomuonaa, pindi tukikutana
Iwe club, kapozi na rafiki zake
Ua tabu, napofikiria ni vipi nimfuate
Muda utafika napo ukweli ntamueleza
Nakosa raha pale washkaji wakinicheka
Sijitambui, nae hajui kama kwake nimefika
Chorus 2x
Bridge
Anavutia
Cha ajabu hajidai
Nataka awe wangu tu, lakini kumwambia ndo siwezi
Chorus