Swahili Song Lyrics of East Africa

Zilipendwa

by Diamond Platnumz

featuring Rayvanny, Harmonize, Mbosso, Lava Lava, Queen Darleen, and Rich Mavoko

Zilipendwa, zama za kale, by Diamond Platnumz of Wasafi Records

Intro 
Ooh, hizo ni zama za kale,
Ohh, sangulo na pepe kalee
Zilipendwa

Rayvanny
Eeh kizamani, kutoa kadi na maua (zilipendwa)
Wanataka mali, ukilipa unakwarua (zilipendwa)
Ufundi kitandani, sio maguvu kujikwamua(zilipendwa)
Unafika ndani, hujatomasa unachanua (zilipendwa)
Wanawake wa leo, wanataka mikakati,
Ukiwa mzogaji, haki ya mungu huwapati,
Mapenzi ya video yatakutoa kamasi,
Eti nikinywa maji, nakuona kwenye glasi (zilipendwa)
Eeh kupiga chabo ghetto (zilipendwa)
Mkono na dettol (zilipendwa)
Sunche na kapeto (zilipendwa)
Majay na Mobeto (zilipendwa)

Diamond
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mmmhh Bolingo ndombolo (zilipendwa)
Twanga chipolopolo (zilipendwa)
Na maji ya kandoro (zilipendwa)
Simba wa Morogoro (zilipendwa)

Rich Mavoko
Mtaani sipati sukari guru kabisa (zilipendwa)
Hivi yuko wapi, Mb Dogg wa Latiffa (zilipendwa)
Babu Tale wapi papa misifa (zilipendwa)
Siku hizi party, hatuendagi Ibiza (zilipendwa)
Mpira na Pele (zilipendwa)
Tanu Nyerere (zilipendwa)
Asha ngedere (zilipendwa)
Alusi mabele (zilipendwa)
Eeti uuze nyumba, ueke heshima bar
Eeti mlazimishe alokukataa
Sabuni kicherema (zilipendwa)
Mabanda ya sinema (zilipendwa)
Lipumba na mrema (zilipendwa)
Diamond na Wema (zilipendwa)

Diamond
Ooh, hizo ni zama za kale 
oooh, sangulo na pepe kale
Wakina Soggy doggi (zilipendwa)
Chaneli ya analogi (zilipendwa)
Movie za cyborgi (zilipendwa)
Van Damme Arnoldi (zilipendwa)

Queen Darleen
Unanibeep nikupigie, umeiweka vocha?
Ule wewe nilipe mie, umeniona lofa?
Tena na madada wenye majina acheni visa
Unaitwa ukale dinner mnakwenda tisa
Nywele za kichina (zilipendwa)
Pochi za kuazima (zilipendwa)
Zena na betina (zilipendwa)
Bashite gwajima (zilipendwa)

Diamond
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mm Amita Bachani (zilipendwa)
TV kwa jirani (zilipendwa)
Madee Rayvanny (zilipendwa)
Zari Ivanny (zilipendwa)

Harmonize
Ya nini kunichunguza naishi wapi (zilipendwa)
Nala chapati kwa mahindi au makapi (zilipendwa)
Kutwa kunikalia una kamati (zilipendwa)
Ooh ya Rabi masikini, kuni dhihaki
Aah Samba mapangala (zilipendwa)
P Funk Kajala (zilipendwa)
Onyango na Jangala (zilipendwa)
Rufufu Mkandala (zilipendwa)
Vya nini vidomo domo, nitupiani tunguli
Kisa pesa za mkopo msimu wa magufuli
Aah Bongoman yondo (zilipendwa)
Sikinde msondo (zilipendwa)
Magari ya udongo (zilipendwa)
Babu wa loliondo (zilipendwa)

Diamond
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Aah TV za kichogo (zilipendwa)
Wakina Man Dojo  (zilipendwa)
Aggy na lyobo (zilipendwa)
Akina Hatupogo (zilipendwa)

Mbosso
Eeti msiba ukiona Bundi unataka kupagawa
Tulale makundi makundi, kuogopa popo bawa
Zuwena ntampata wapi (zilipendwa)
Zueena wa zile nyakati (zilipendwa)
Kujifanya mapanga sunna eti wamepinda
Wengine wabeba vyuma na hakuna marinda
Iddi Amini dada (zilipendwa)
Miuno ya H Baba (zilipendwa)
Domo Chai Jabba (zilipendwa)
Michezo ya kibaba baba (zilipendwa)

Lava Lava
Wale wapiga madeal, sasa hali mbaya (zilipendwa)
Hizi zama za magufuli, si za jakaya (zilipendwa)
Ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya (zilipendwa)
Vikatuni vya madenge baba ubaya (zilipendwa)
Muhogo mchungu Mr. Bean, wapi bambo
Wale wazamiaji wa melini, wazee wa ng’ambo
Hivi yuko wapi Benjamini wa Mambo Jambo
Wa Vietnam waporini vita na Rambo 
Eh ndanda Mjela jela (zilipendwa)
Kidali kombolela (zilipendwa)
Max na Zembwela (zilipendwa)
Juma Nature na Fela (zilipendwa)

Diamond
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mmmh kamanda Daz Nunda (zilipendwa)
Kalumanzila ndumba (zilipendwa)
Simu za dole gumba (zilipendwa)
Johari na Kanumba (zilipendwa)