Swahili Song Lyrics of East Africa

Iveta

by Sajna

Intro
Oh ooh, ey ye ye yo yoooohh
Oh oohh, we Iveta
ningojee dia, ningojee dia
tetemesha, bwoy
Verse 1
Najua moyo wako unahitaji raha, ila huku mjini karaha
baridii inaumizaa, wewe sweta ulileta mzaha
sijui jibu langu umepata, kuhusu Saj kuja kwenu kukubaliwa
isije kuwa hadithi na ndoto, walishanieleza mapenzi maji ya moto
najua kwamba unanipenda mimi
ubavu wa kushoto ningoje Iveta.
Chorus
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Iveta kijijini ningojee mamaa, ningojee dia
huku mjini nakutafutia mama, nakutafutia dia
Verse 2
Subira yavuta heri, nisubiri kwa kila lakheri mpenzi
kijijini nimemiss vitu vingi, mboga za majani machungwa matunda
pale nyumbani hadithi za babu, ndugu zangu na utani wa bibi
Iveta nisubiri mimi, tuunganishe familia yangu na yako
Iveta maa, i love u
Iveta maa, i need you
Iveta maa , i love you.
Repeat Chorus
Bridge
Eeh eh ehh eh, ningojee dia
Aah ah ahh ah, nakutafutia dia
Verse 3
Mjini sichoki kutafuta, angalau senti kuja kuzileta
Iveta nisubiri basi mimi, si unajua nakupenda sana wewe
wangapi huku mjini wanitaka, ila najua wewe ndio unaningoja
usiwe na shaka ningoje mama, Iveta wewe (3x)
Repeat Chorus
Outro
eh eh eh eeeeh, haa
oh ooh, ningojee dia wange
ningojee diaaaaaaaaaah, haaa
tetemesha, bwoy