Swahili Song Lyrics of East Africa

Kupanda na Kushuka

by Nikki Mbishi

featuring Lady Jaydee, One the Incredible, and Songa

kupanda-na-kushuka-nikki-mbishi-one-songa-lady-jaydee

Tamaduni muzik (yeah)
Combination sounds
Combinenga
 
Chorus (Lady Jaydee)
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
 
Verse 1 (Nikki Mbishi)
Vaa wema vua shari safari hatua, 
Round hii mbishi niko gengeni na jua kali, 
Siuzi nyanya vitunguu wala pilipili hoho, 
Too little too late ushachelewa Jojo, 
Wakiniona mi nashine wanachonga, 
Ndo maana kila line wanaponda, 
Vipi nikisign na Anaconda, 
Busy kwenye show mi nashow biz na kwa flow hizi si ndo time ya kusonga, 
Hahahahaaa!!! hii ni hit ya kubaki, 
Mwenyei kaniumba fit ndo maana lift sitaki, 
Nabang kila session mpaka morning groove, 
Eti niko chini hunioni juu?,Mi ni leader wa performing crew, 
Nizungue ubaki mweupe design ya hair style ya Monikuu, 
Haah Nikki Mbishi Songa One The Incredible, 
Komando Yosso ni mzozo ngoma ni terrible, 
Karibuni.. 
 
Chorus (Lady Jaydee)
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
 
Verse 2 (One the Incredible)
Wanasema wanapenda vile mi hubonga kila kitu, 
Rap sonara madini huwa nachonga kila siku, 
Sina fleva za kibongo naonja kila kitu, 
Bila woga wanaloga niwe kioja kila siku, 
Kama unaipenda push play ama itose, 
Everyday iwe kush nei ama okay, 
Wazushi msichoke naghushi ninyooshe, 
Nipe changamoto sio kila nikigusa tu okay 
Kuna watu wangependa nigote kwenye misele, 
Iwe kwere kote Moko nisote nisiende mbele, 
Nichoke niwe kero kokote au niende selo nisitoke, 
Ila msiogope nipo milele, 
Kwani muumba ndo mpaji kutunga kipaji, 
Niko macho wanataka kuniua niwe mtaji, 
Niko Anaconda na hii ndo ile siku niko macho, 
Ila wengi watakesha kila siku
 
Chorus (Lady Jaydee)
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
 
Verse 3 (Songa)
Chungu kichungu natema sumu kisumu, 
Hali ni mgumu je utabeba dumu kidumu, 
Na kidumu mpaka wasaa utapotambaa, 
Na kushangaa kwamba kufika humu ni ngumu, 
Ukicheck chance hola,unawaza utaishi vipi endapo majambazi wakipora, 
Basi bora,kuwa na wasi kama polisi ni sawa na wazazi wenye bastola, 
Heeey.. na bado utakosa njozi,kazi hakuna utanuna utashona gozi, 
Niite Songa endapo utakosa pozi, 
Au nyong'onyea zaidi ya mgonjwa aliyekosa dozi, 
We si kiongozi – ndio, 
Mbona maji hakuna wananchi mtaani wanaoga chozi
 
Chorus (Lady Jaydee)
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho
Siku ikifika tukubali, tuwe macho 
Kupanda na kushuka zote hali, tuwe macho