Swahili Song Lyrics of East Africa

Machoni Kama Watu

by AY

featuring Lady Jaydee

Chorus
Machoni kama watu
Mioyoni hawana utu
Imani imetoweka
Mabaya yanaongezeka x4

Verse 1
Wengi wao wanatabasamu, wanaongea kwa nidhamu
Wanajifanya watu wa karib kumbe hao ndo sumu
Wameweka mbele dini fungo moyo usiwaamini
(Si unakumbuka alikufaa kwa dhiki)
Kweli
(Enzi zile upo nae marafiki)
Aha, yuko wapi sasa hayupo tena ashasaliti
Kweli akufaae kwa dhiki mara nyingine ni msaliti
Alishatembea na mkeo kwa gia ya urafiki
Shoga yako kwako habanduki mmeo akakutaliki
Unajuta ye anacheka kwani ndoa keshaivuruga
Mmeo ametimua ye keshatawala nyumba
Baba na nyumba ndogo watoto wanalia mateso
Anadiriki hata kuwakana hana huruma hata kidogo
Haina mshangao watu wa aina hii wapo
Sio sehem zingine hata hapa ulipo wapo
Jirani yako mchana mnacheka usiku mwanga
Nia yake kuona life oh inapinda
Dili zote zigime mipango igonge mwamba afya yako
Bandika bandua ya magonjwa itatamba……

Chorus

Verse 2
Yoh! dunia inavunda vvu walimwengu hawashikiki
Wengi wanapenda ngono lakini kuzaa hawataki
Wengi nacheka nao tu lakini sio kwa dhati
Hivyo ni kama nipo gizani halafu nalamba ncha ya mkuki
Wengi wanatoa mimba wengine wanatupa watoto
Ungekuwa wapi mama yako angekutupa enzi hizo
Imani hakuna ndani ya maovu yasio na mwisho
Nakata tamaa akili inachoka moyo mzito
Machoni kama watu kumbe wamejaa unyama tu
Kaa chonjo chunga sana napo akili kichwani tu
Hapendi kukuona unatesa juu yako mzigo chuki
Ameshatega mabaya mitego ndo haikamatiki
Hapendi kuona unawini hapendi kuona unafuraha
Raha yake kuona umezungukwa na karaha
Hana raha anapoona mambo safi kiuchumi
Moyo utakuwa shwari tu pale una hali duni

Chorus

Verse 3
Huyo ndo mwanadamu anapowini tu dharau
Napo ni mgumu kuelewa mwepesi kusahau
Anajionyesha ana huruma,mpole na mkarimu
Na aliye mstari wa mbele kutoa ahadi tamu
Usimpa nafasi hata ajue zako habari
Hana jema chunga sana hana ujio wa heri
Hataki kabisa kuona unavuta hewa hii lakini
Wapi mipango inabaki zzzzz!!
Ni rahisi kwake kupata mali kwa njia ya kuua
Haya mambo hi hali nadhamni wote mnaijua
Mlale pema mliouwawa mkidai zenu haki
Sisi bado tupo duniani hatujui lini tamati
Jasho la mnyonge huwa ni neema kwa wachache
Ni kilio cha fukara chenye lengo haki nipate
Stuka huko tunakokwenda kunatisha
Kwani itakuwa ndoto watu kutenda mema kabisa

Chorus