Swahili Song Lyrics of East Africa

Mikono Juu

by AY

Intro
Let me talk to ya!
Nataka kusema sana (No si sana)
kuhusu watu wa aina fulani, mzeiya A-Y sema

Chorus
Mikono juu, onyesha kama hufagilii mambo ya kishamba (4x)
Ha juu! Nyosha mikono ishara tumewapiga bao (4x)

Verse 1
Yatazame vyema macho yangu right now
Nishapitia mambo mengi hata zaidi yao
Unapongata kwangu na kupulizia kwao
Unapochoka zaidi baada ya kuona mi nacheka nao
Oh
Leo nakupa ukweli baada ya kuona unanispy
Oh
Cheza nami mbali sitaki hata unisabahi
Sikujui
Niaje nipoteze muda nikuchunguze
Hunijui
Vipi utunge uzushi kwangu uyasambaze
Mind your business hujui style ya Maisha yangu
Basi sitaki ubishe hadi kwenye anga zangu
Kila siku unayafuatilia, nayoyahangaikia
Lakini huwezi kuniharibia
Usione nimeshhh ukataka kupima
Nilikuona mwema kumbe zzzz nishakusoma
Nikiwepo mtu poa, nikiondoka unanichoma
Sasa unapochoma kama unaoga nje mchana ah
Niko imara zaidi ya chuma cha pua
Sitabiriki ujio wangu moyo wako unajua
Mlango wa ngome yangu mjomba noma ngumu kuingia
Ndo maana bado mi nakamua border nyingi napasua

Bridge
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
Hoya (2x)
Hoya (2x)

Repeat Chorus

Verse 2
Usione watu wamechill wametulia, busy
Basi ukaona easy kuwachezea, ukidhi
Kupandikiza chuki news kudandia please
Sitaki lawama kama vipi we potea
Fanya usepe tu kwangu, kwangu hupati kitu fool
Niogope kama OGOPA full wa mbuzi kama FID Q
A Y (2x)
Bado nafanya mema huu
Nikipata, nikikosa namshukuru Mungu tu
Kikulacho mbona kinguoni mwako
Wanaokuua mbona wa karibu yako
We unashangaa nani anauza file lako
Kama Adili kama mi (Bora niwe peke yangu)
Deal zako ka zinabuma basi hasira usilete kwangu
Kama zali oh si lako jitume kibingwa wangu
Sio unakaa tu, kazi tu, kupiga majungu
Napo muda unapata bado unapiga virungu

Mchawi hana alama wapo (humuhumu)
Asiyependa uendelee ni (mchawi tu)
Hakosi uja kwako hodi kila saa (ngo,ngo)
Ndani chuki nje kila saa anakupa tano (ngum, ngum)

Bridge
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
Hoya (2x)
Hoya (2x)
Bridge
Shida zangu kwani zinakuhusu nini (wewe)
Hata raha zangu zinakuhusu nini (wewe)
Pia Maisha yangu yanakuhusu nini (wewe)
Hoya (2x)
Hoya (2x)

Repeat Chorus

Bridge
Aah ah
Usijaribu kuchunguza sura hii
Aah ah
Kama ina raha ama zzzz
Aah ah
Usilete tabia za kizamani
Maisha yangu yanakuhusu nini

Outro
Au vipi bwana, ni hayo
Huu ni muda na kila mtu kujiheshimu rafiki yangu
Haijalishi wewe ni nani na unatoka wapi
Niachie mimi nifanye kama mimi
Sababu siwezi kufanya kama wewe na wewe huwezi kufanya kama mimi
Sikiliza Ambwene, hili ni bonge la dude
Bonge la beat kutoka kwa OGOPA
Matrack kama haya yanatakiwa kusikilizwa mtaani
Chuki kibao zipo, kwa nini?

Usichukulie poa! (2x)