Mafunzo yote
by Banana Zorro
Mafunzo yote! Pozi zote! Mauzo yote!
Eti binti hanitaki
Nimesubiri sana, nimechukua za uso, kuda deki!
Si uzoba huu? Aiyey!
Chorus
Subira yangu ndiyo iliyoniponza
Ngoja, ngoja, naonekana Zoba
Subira yangu ndiyo iliyoniponza
Ngoja, ngoja, naonekana mjinga
Kwa sababu nilimpenda kweli (4x)
Verse 1
Mawazo, mawazo yatawala kichwa changu, ee
Maumivu, maumivu yamevunja moyo wangu ee
Kusubiri, kusubiri, nimekusubiri mpenzi wangu ee
Lakini umekuja kuuvunja moyo wangu ee
Nilikuwa nikamili nisifanye jambo lolote nawe
Mpaka tuje tufunge ndoa, umalize na masomo
Huko umekwenda huko chuoni ee
Umebadilika mama, umebadilika, umebadilika sana
Mama yo, mama yo
Mama yo, mama yo, mama yo
Unaniona mimi Zoba, Zoo-oba ee
Chorus
Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Imeniponza miye ee)
Ngoja, ngoja, naonekana Zoba (Zoba la mapenzi ee)
Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Nimepotezwa miye ee)
Ngoja, ngoja, naonekana mjinga (Sijui la kufanya ee)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Kweli eee)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli ooo)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Mama yo, mama yo)
Verse 2
Inauma sana, mpenzi wako
Wampenda sana, wamlinda sana,
Wapata habari, kumbe mwenzako
Kampenda sana, rafiki yako
Ndo maana juzi, umeacha mazoezi
Ndo maana siku hizi hutaki kuwa na mimi
Mapenzi (mapenzi) yananiumiza (yananiumiza)
Mapenzi (mapenzi) yananitesa (nitakulinda wewe)
Maumivi ya mapenzi, zaidi ya mwiba
Sikitiko la mahaba, la shinda msiba
Nitakulinda mama
Nitafanya jambo lolote kwa ajili yako nahakikisha nakuwa na wewe, wewe ee
Mama yo, mama yo, mama yo
Unaniona mimi Zoba, Zoo-oba ee
Chorus
Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Imeniponza miye ee)
Ngoja, ngoja, naonekana Zoba (Zoba la mapenzi ee)
Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Nimepotezwa miye ee)
Ngoja, ngoja, naonekana mjinga (Sijui la kufanya ee)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Kweli ee)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli ee)
Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli oo)
Kwa sababu nilimpenda kweli
Mama yo, mama yo (3x)
Nitakulinda wewe, mpenzi wangu wewe
Hii ni ahadi naiweka kwako wewe
Wewe oo, wewe oo
Upo kwa ajili yangu ee
Nitasubiri siku zote
Litunze penzi langu mama
Mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi mabaya
Mapenzi mabaya, mapenzi mabaya, mapenzi mabaya, mapenzi mabaya
Lakini mpenzi wangu, mapenzi, umalize masomo tuwe wapenzi kweli
Tufunge ndo na we mama nakupenda
Nakupenda kama wali wa nazi (I love you)
Mbona mwenyewe,
Nimeamua kusubiri oo, kusubiri
Usifanye mama, nikaonekana Zoba
Nikija kungoja, siku zote mama