Swahili Song Lyrics of East Africa

Mama Kumbena

by Banana Zorro

Chorus 2x
We mama kumbena, we mama kumbana
We mama kumbe mama kumbe mama kumbena

Verse 1
Mara ya kwanza ulipokataa mahari yangu
Nilidhani labda sababu kazi yangu
Mara ya kwanza ulipokataa posa yangu
Aliniumiza na kutesa moyo wangu
Ndipo jirani zake wakaniambia
Ni kawaida yake na wengi kawakatalia
Ndipo jirani zake wakaniambia
Ni kawaida yake na wengi kawakatalia ah

Repeat Chorus 2x

Verse 2
Mama kumbena wowowo ah hah ha
Wooo ahhh ahh weee mama kumbena
Wooo yeeah wewe mama kumbenaa

Siwezi sema sababu ni mali
Maana kashakataa mpaka matajiri
Naweza sema sababu hakubali
Binti kashakuwa kiumri kiakili

Wee mama kumbenaa
Siamini nilichosikia
Hutaki kumwoza Binti, kisa umemzoea
Wee mama kumbenaa
Siamini nilichosikia
Hutaki kumwoza Binti, kisa umemzoea

Repeat Chorus 2x

Bridge 4x
Tunaleta posa hata kama ukitutosa
Tunaleta posa hatutaki kumkosa
Ayayayaya
Kumkosa kumbena ni ngumu naona
Kumkosa kumbena sababu nampenda sana
Kumkosa kumbena
Kumbena ah yeyeyeyeyeye
Repeat Chorus and Bridge till fade