Swahili Song Lyrics of East Africa

Mwana

by Alikiba

Mwana by Ali Kiba, Tanzania

Mali ni nyingi nyumbani kipi kimekukimbiza
Ona babio mamio wote wanakulilia
Mtoto peke yako nyumbani kipi kimekukimbiza
Ona babio mamio wote wanakulilia
 
Ndani ya Dar Es Salaama ulikuja bure
Tena kimwana kimwana hujui kuchuna
Na zile lawama za wale walokuzoeza
Ulikuja jana na leo tofauti sana
 
Tena bora yule wa jana wa leo tofauti sana
Dakika mbili mbele nyuma kichwa kinauma
Tena bora yule wa jana wa jana leo wa jana
Dakika mbili mbele nyuma kichwa kinauma
oyayee
Mbona unawatesa sana?
omamee
Mbona unajitesa sana?
 
Ukaanza kulewa madawa kuvuta kwa sana
ndani ya Dar es Salaam mambo matamu hayakukuisha hamu
we bado mtoto kwa mama hujayajua mengi
Mwenda tezi na omo marejeo ngamani
 
Amesema sana mama dunia tambara bovu
kuna asali na shubiri ujana giza na nuru
We mwana wewe mwana, mwana jeuri sana
Ulichokifuata hukupata, umekosa ulivyoacha
 
Kwa baba yako mwana na mama yako mwana
Kwa vichache ulivyovitaka ni vingi ulivyoacha
oyayee
Mbona unajitesa sana?
omamee
Mbona unawatesa sana?