Swahili Song Lyrics of East Africa

Pepea

by Benjamin wa Mambo Jambo

Verse 1
Chambichambi zilinitoka,ukajifanya kunitoroka
Kama ndege ukaruka,wenye fedha wakakuteka
Ndoto zangu zote zikaishia hewani,nikabaki na jeraha moyoni
Watu wengi wakacheka sana kwa sababu,nilibakia kama hayawani
Ulidhania siwezi tena,kuishi peke yangu
Ukafikia kiwango chaku-mtusi mama yangu
Ukaniona sifai tena,eti huzioni pesa zangu
Wale watu walikudanganya,umevunja moyo wangu
Vipi mbona tena unataka kurudi tena nafasi zimejaa
Ulipokwenda wamekutema,unataka kurudi nyuma(hebu muogope jah)
Wakurugeta wameshapita,nilidata ukanitosa(nilikuwa majalala)
Waweza kwenda ulipokwenda kwani bado nakidonda(unapigwa na butwaa)

CHORUS
Fly( toka zako),fly(nenda zako),like a butterfly(oooh oooh)
Fly (toka zako),fly(nenda zako),like a butterfly
Yeeeh oooh,pepea hee,potea hee
Yeeeh oooh,pepea hee,potea hee

Verse 2
Nilikupenda kama papai,nikakulea kama yai
Lakini bado hukujali,ukawafata wenye mali
Nikapita kona zote nakusaka,kumbe ulishakimbilia mbali
Hadi kwenu nilikuja kuuliza, ila ndugu zako hawakujali
Wakasema kwamba sina pesa,siwezi kukuposa(hee)
Moyo wangu ukautesa,nilikumiss nikakukosa(hee)
Watu wengi wakanicheka,wakasema nimedata(hee)
Muda mwingi umeshapita ,ndio unarudi kunisaka
Toka sikuhitaji tena,tena ulijifanya msapinapi
Waliokupenda wako wapi,umeshalala na wangapi
Umegawa tunda kama pipi,usinibeep sibipiki
Moyoni kwangu sina nafasi wala sijui nitakuweka wapi

CHORUS

BRIDGE
Aaah say goodbyeee,yeeeh oooh,heee mmh
Pepea hee,potea hee,pepea hee potea hee
Pepea hee,potea hee,pepea hee potea hee
Pepea hee,potea hee,pepea hee potea hee
Pepea hee,potea hee,ndio maana yake!

CHORUS