Swahili Song Lyrics of East Africa

Shika Adabu Yako

by Nay Wa Mitego

Shika Adabu Yako by Nay Wa Mitego, including Swahili Lyrics

Intro
Wanabebwa na refa na bado nacheza rafu
Mi siogopi kufa, ngoja kwanza nipige pafu
Sss, ehe-hee pumbavu!
Wapinzani wajipange round hii ni ligi ndefu
 
Haya najisikia kuwachana (wachane)
Niwachane? (Wachane!)
Najisikia kutukana (watukane)
Eh, niwatukane? (Watukane!)
 
Verse 1
Haya naanza kuchana, kuhusu wasichana
Hawa ndio mama zetu ila sometimes hawana maana
Wapo wanaofanya mziki na mziki hauwalipi
Dada zetu wa mjini siku hizi hawavai chupi
Najiuliza ni joto au fashion
Au biashara ndo wanafanya promotion?
Aliokanja nikanjue, niwachane hawa ma-boy
We ni moto uliyewashwa, usiyezimwa hata kwa fire
Bongo Movie imekufa wamebaki kuuza sura
Wote wanataka kuimba ka Shilole na Snura
Ray Kigosi kawa mkongo hadi leo anaishi kwao
Hela za kuuza movie zote ananunua mkorogo
Kama ni umri umeshaenda, au bado anajiona dogo?
Diva Supermario, ana gari ya milioni 10
Hajawahi miliki ghetto
Anaishi tu kwa mademu, gari lake ndo ghetto
Huu ndio wendawazimu!
Kumiliki gari sijui ndo yake ndoto!
Mnaopanga kunishitaki nawapa dole la kati
Mkashtaki hata kwa Magu na bado ntawapa facts
Si wamekuchagua wenyewe Magu waonyeshe maujuzi
Vunja mpaka ikulu wakikuletea upuuzi
Aah! Sifanyi beef mimi na watoto wa juzi
 
Chorus
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
 
Mi sitaki tugombane
Nia nikurekebishe, haya mambo yaishe
Mi sitaki tugombane
Nia nikurekebishe, haya mambo yaishe
 
Bridge 1
Nataka kwenda Msanga, oh nauli na bure
Chakachaka, chakachaka, oh nauli na bure
Nataka kwenda Msanga, oh nauli na bure
Chakachaka, chakachaka, oh nauli na bure
 
Verse 2
Kama ni vumbi litaruka na mikia watafyata
Hizi taarifa zangu na ziwafikie BASATA
Nyie ni kuku au bata? Msumeno usiokata
Kazi kufungia nyimbo, mnajua shida tunazopata?
Hamjui wajibu wenu, mngekuwa watoto nshawachapa
Na Mungu hakunyimi vyote lazima atakupa chako
Demu ana sura mbaya ila ana bonge la tako
Na wasanii wadananda, ila Shetta kazidi
Huyo ndo baba Qaila (okay!)
Gari kapewa na Chief Kiumbe utasikia, “my new ride!”
Kwenye kazi ongeza bidii
Maadui ni wengi ongeza speed
Ah, siku hizi kusoma chuo, wala sio sifa tena
Ni kama maonyesho ya urembo, miksa na u-modal
“Dada unafanya kazi gani?”
“Mi mwanafunzi wa chuo”
“Kila siku uko batani!”
“Ndo maisha yetu wanavyuo”
 
Chorus
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
 
Mi sitaki tugombane
Nia nikurekebishe, haya mambo yaishe
Mi sitaki tugombane
Nia nikurekebishe, haya mambo yaishe
 
Bridge 2
Haya ni ruksa, kunyonga kidogo nipe cha Arusha, hey
Naongea na pusha, mzuka umepanda mbona unanirusha?!
The True Boy is in a building!
 
Verse 3
Tushazoea wasanii ndo watu wanaopenda kiki
Ila round hii, ligi serikalini
Hii serikali ya “Kazi Tu”, kwani inaendeshwa vipi?
Kila kiongozi ana muandishi, wanashindana magazetini
Huyu jamaa anajiita Dimpoz, Pose kwa Pose
Wanae wanalalamika hawamjui shemeji
Kitaani kuna tetesi mwana hapigi mechi
Mara oh jogoo hawiki, huwa haonyeshi shemeji
DJ Choka daily bata, hivi hauna familia?
Nasikia hata nyumbani huna godoro la kulalia
Wema Sepetu una mimba kweli, au ndo kiki za msimu?
Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu
Na siku hazigandi tayari ushakuwa bibi
Na unakoelekea utatafuta kiki hadi kwa Fid
 
Chorus
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
Haya wewe, haya wee
(Shi-shi-shika adabu yako!)
 
Outro
Haya ni ruksa, kunyonga kidogo nipe cha Arusha, hey
Naongea na pusha, mzuka umepanda mbona unanirusha?!
The True Boy is in a building!
 
It’s a 966, baby
Free Nation