Hakuonekana na binti
by Mwana FA
featuring Lady Jaydee
VERSE I
Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini
Mfuasi mzuri wa maadili lakini alikufa kwa ngoma
Aliwarudisha waliopotea akawapa tiba mbadala
Na adui mkubwa wa zinaa lakini alikufa kwa ngoma
Najaribu kumjengea picha mshkaji alie kalala ndani ya futi 6
Namkumbuka mtaani mtaani alipokuwa anakatisha
Na mara kadhaa maskani washkaji ungemkuta
Usingedhani ana ngoma machoni alivyokuwa mwema (alivyokuwa mwema)
Mzuri, mtanashati aliyewaza kabla ya kusema
Ibilisi wa njaa za mwili daima alimchezea mbali
Tungi, vicheche, mineli hakuonekana kujali
Tazama maisha yake hutaliona kosa lake
Kama aliyefunga kufuli kati kati ya nyeti zake
Mkali wa ushauri nasaha aliyeongea kuhusu mapenzi huku akipinga zinaa
Ungesema achague kipindi angechagua njia panda
Nyumba aipendayo angechagua ya ibada
Utepe mwekundu mpaka kwenye nguo zake za ndani
Nadhani mimi najali wewe je?
Kama alikufa kwa ngoma jiulize alijali nini!
CHORUS
Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini
Mfuasi wa maadili (Lakini alikufa kwa ngoma)
Alirudisha waliopotea akwapa tiba mbadala
Adui wa zinaa (lakini alikufa kwa ngoma)
VERSE II
Mara nyingi alikuwa mpole mara chache alizoongea wote tulimgeuza shule
Nasaha za bure kama tupo class vile akatuasa kuhusu kuhusiana
Akatuonya kutoaminiana mtazamo wake na wa-mama Terry daima ulifanana
Hadithi ya maisha yake ilikuwa safi kama ya Nabii
Hakuna aliyeamini mwisho wa mshkaji utakuwa namna hii
‘Gawa sana condom na kufunza kama angaza
Vijarida vya Ukimwi ye’ndio alikuwa msambaza
Ina maana alikuwa anatoa bila vyake kubakiza
Ama amekuwa ufunuo mola anaonyesha miujiza
Tazama siku zinakata hatumuoni nini kasoro
Afya yake haieleweki eti imeanzisha mgogoro
Leo anadunda kesho mgonjwa na hataliacha godoro
Labda alifanya kwa siri hadharani hakuna shahidi
Labda alivumilia sana mwisho kuasi kukambidi
Hatujui! hatuwezi sema na bado tunashangaa
Vipi vipimo vinasoma mshkaji alikufa kwa ngoma
CHORUS
Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini
Mfuasi wa maadili (Lakini alikufa kwa ngoma)
Alirudisha waliopotea akwapa tiba mbadala
Adui wa zinaa (lakini alikufa kwa ngoma)
VERSE III
Sijaribu kuibadili nyekundu kuwa njano huu ni mfano
Kwamba Ukimwi ni kwa wote wembamba na wacheza sumo
Wazinzi, wema pia wamo na hauji kufuata kimo
Ungedhani yupo salama kuzidi usalama wenyewe
Ungedhani ukimwi utaogopa utamuacha mshkaji mwenyewe
Sivyo! Haufanyi utakavyo wewe unafanya utakavyo wenyewe
Hakuonekana ana binti hakuwahi kuiahasi dini
Mfuasi mzuri wa maadili “Lakini alikufa kwa ngoma”
Amsha akili janga kangha gani ulibebebee
Siwaambii msiusie sisemi zipu mfungue
Sisemi muache kuwa wema ila ujinga usiendelee
Kwamba kila anayekufa kwa ngoma msidhani kicheche
Tuamini bado ni wenzetu msiache wagonjwa wajifiche
CHORUS
Au sio, tumeelewana naamini, tusihukumu
Hatuna hakina kuwa waathirika wana hatia
Tusiwanyenyepaee…..aaight!?